SOS yakabidhi Bima za afya kwa watoto 71 Pemba.
MSAIDIZI Mkurugenzi wa huduma za kijamii na afya ya Msingi kutoka Baraza la Maji Chake Chake Dk.Moh’d Ali Jape, amesema anasikitishwa na baadhi ya wazee kurudisha nyuma juhudi za serikali pamoja na mashirika mbali mbali yanayojitokeza kusadia huduma za afya kwa watoto.
Alisema kumekua na baadhi ya wazee wanashindwa kuwapeleka watoto wao hospitali kupatiwa huduma ya afya, kwa kisingizo cha kutokua na nauli au kujali kwenda shamba kulima, wakati mashira hayo yameshatoa fedha nyingi kwa ajili ya kuwahudumia watoto hao.
Hayo aliyaeleza huko skuli ya sekondari Vitongo Wilaya ya Chake Chake, wakati alipokua akikabidhi kadi 44 za Bima ya afya kwa wazazi na walezi wanaolea watoto ambao wamo katika mradi wakuimarisha familia unaotekelezwa na shirika la SOS Pemba.
Aidha aliwataka wazee ...