RC Ayoub azindua kikundi.
MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Ayoub Mohamed Mahamoud, amewataka vijana kisiwani Pemba kujiendeleza kitaaluma katika fani mbali mbali, ili wawe na uwezo wa kuzitumia fursa za mabadiliko makubwa ya kiuchumi pale zitakapokuwa tayari kutekelezwa.
Alisema tayari serikali imesha karibisha wawekezaji tofauti kuwekeza kisiwani Pemba, kwa lengo la kuimarisha uchumi wao, hivyo haitokuwa jambo la busara kuona fursa za ajira zinapotokea katika makampuni vijana wa YCCG wanashindwa kuzitekeleza.
Alifahamisha kuwa kumezoeleka vijana kukaa mitaani baada ya wawezekaji kuwekeza, na kutangaza ajira waza wanabakia nyuma na ajira hizo zinachukuliwa na wageni.
“Mimi katika mkoa wangu ajira nyungi tena muhimu katika mahoteli zimechukuliwa na wageni, wazawa ...