Wahitimu 51 wa Skuli ya Ng’ambwa watunukiwa vyeti.
WAZAZI na Walezi wameshauriwa kutumia lugha nzuri kwa walimu wakati wanapotakiw akufika skuli, pamoja na kufuatilia mienendo ya watoto wao kielimu.
Ushauri huyo umetolewa na aliyekuwa Afisa Mdhamini Wizara ya Vijana Utamaduni sanaa na Michezo Pemba Fatma Hamad Rajab, wakati alipokuwa akizungumza na wazazi, walezi na wanafunzi wakati wa mahafali ya 13 ya skuli ya Sekondari Ng’ambwa Wilaya ya Chake Chake.
Alisema mashirikianao mazuri baina ya wazazi, walezi na walimu ni jambo zuri linalopelekea wanafunzi kusoma kwa bidii, kwani kila mmoja anakuwa tayari kusimamia suala la elimu.
Alifahamisha kwamba wazazi wanaposhindwa kufuatilia mienendo ya watoto wao, basi watoto hao hupelekea kufanya vibaya katika mitihamnbi yao, pamoja na kuwa na maendeleo mabovu ya elimu skulini hapo.
Ai...