Thursday, October 31
Mahafali ya 10 ya skuli ya maandalizi Star  yafana.
Michezo

Mahafali ya 10 ya skuli ya maandalizi Star yafana.

  MKURUGENZI wa Elimu ya Msingi na Maandalizi kutoka Baraza la Mji Chake Chake Makame Pandu Khamis, amewataka wazazi au walezi kuhakikisha wanaitekeleza kwa vitendo mikaba wanayopewa skuli, wakati wanapokwenda kuwaandikisha watoto wao ili kuepuka migogoro inayotokea baadae. Alisema kumekua na tabia ya wazazi kutokuifuata kimilifu mikataba hiyo, baada ya watoto wao kukubaliwa katika skuli walizowapeleka. Mkurugenzi huyo aliyaeleza hayo wakati wa mahafali ya 10 ya skuli ya maandalizi Star Nursery school iliyopo kichungwa Wilaya ya Chake Chake, pamoja na kuzungumza wazazi na walezi wa watoto. Alisema iwapo wazazi watashindwa kutekeleza kwa vitendo mikataba wanayopewa skuli, skuli hizo zitakosa maendeleo ikizingatiwa hazina bajeti wala ruzuku kutoka serikalini. “Niv...
NMB yakutana na wakulima wa mwani na chumvi.
Biashara

NMB yakutana na wakulima wa mwani na chumvi.

  Benk ya NMB Kisiwani Pemba, imekutana na wakulima wa zao la Mwani na Chumvi katika shehia ya Kiungoni na Mjini Kiuyu, kwa lengo la kujua changamoto zinazo wakabili wa kulima hao. Wakizungumza na wakulima hao kwa nyakati tafuti, uongozi wa NMB umesema lengo ni kujuwa changamoto zinazowakabili na kuona jinsi gani wanaweza kuwasaidia. Meneja Mwandamizi kutoka idara ya kilimo na biashara Bank ya NMB Tanzania Wogofya Mfalamagoha, alisema NMB ni miongozi mwa mabenk yaliyopiga hatua kubwa Tanzania, huku ikiwa mstari wambele kusaidia katika sekta ya kilimo, uvuvi. Alisema katika kuelekeza nguvu zao kama benk, imeakua kuanza na wakulima wa mwani na chumvi, kwani ndio wakulima wanaopata tabu kutokana na vilimo vyao. Wogofya alisema wakulima wa mwani na chumvi huwapatia ...
Waziri Jamal atoa maagizo Pemba.
Biashara, Kitaifa

Waziri Jamal atoa maagizo Pemba.

  WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Jamal Kassim Ali, amemuagiza Mkandarasi kutoka kampuni ya ADVENT Construction Limited wa mradi wa ujenzi wa jengo la ofisi za ZRB Gombani, kuhakikisha anaongeza wafanyakazi pamoja na kufanya kazi usiku na mchana, ili liweze kumalizika mwishoni mwa mwezi huu. Jamali alitoa agizo hilo baada ya kutembelea ujenzi wa mradi huo wa ujenzi wa ofisi za ZRB Gombani Wilaya ya Chake chake, na kusikiliza maendeleo yake akiwa katika ziara yake ya siku mbili ya kutembelea miradi na taasisi mbali mbali zilizomo ndani ya wizara hiyo. Alisema Mkandarasi huyo anapaswa kuajiri wafanyakazi kutoka kisiwa cha Pemba, kwa ajili ya upakaji wa rangi na matengenezo ya mwisho, ili kati kati ya mwezi huu atakapokuja tena kukagua kazi hizo zi...
Dk. Hussein Ali Mwinyi ameupongeza utayari wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) wa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Awamu ya Nane.
Biashara, Kitaifa

Dk. Hussein Ali Mwinyi ameupongeza utayari wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) wa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Awamu ya Nane.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dk. Hussein Ali Mwinyi ameupongeza utayari wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) wa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Awamu ya Nane katika kuimarisha sekta mbali mbali za maendeleo na kukuza uchumi wa nchi. Rais Dk Hussein Mwinyi ameyasema hayo leo Ikulu Jijini Zanzibar wakati alipofanya mazungumzo na Uongozi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), ukiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo Theobald Sabi akiwa amefuatana na Meneja Uhusiano William Kallaghe na Ramadhan Lesso ambaye ni Meneja wa Tawi la NBC Zanzibar. Katika maelezo yake Rais Dk. Hussein Mwinyi aliueleza uongozi huo kwamba amefarajika kwa kiasi kikubwa na utayari wa Benki hiyo katika kuunga mkono juhudi za Serikali na kusisitiza kwamba mash...
Dk. Hussein Ali Mwinyi ameitaka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuhakikisha Vyama vya Michezo vinakuwa na utaratibu maalum utakaowezesha wafanyabaishara kujitokeza na kudhamini michezo.
Kitaifa, Michezo

Dk. Hussein Ali Mwinyi ameitaka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuhakikisha Vyama vya Michezo vinakuwa na utaratibu maalum utakaowezesha wafanyabaishara kujitokeza na kudhamini michezo.

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ameitaka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuhakikisha Vyama vya Michezo vinakuwa na utaratibu maalum utakaowezesha wafanyabaishara kujitokeza na kudhamini michezo hiyo. Dk. Mwinyi amesema hayo Ikulu Jijini Zanzibar, katika hafla ya makabidhiano ya fedha zilizotolewa na Wafanyabiashara watano wa Zanzibar kwa ajili ya ushiriki wa Timu ya Mlandege, kuelekea mchezo wa marudiano dhidi ya Timu ya CS Sfaxien ya Tunisia. Alisema maendeleo ya michezo hapa nchini yatafikiwa kwa kuwepo udhamini  wa uhakika utakaozinufaisha pande zote mbili kati ya wafanyabaishara na vilabu. Aliwataka wafanyabiashara kote nchini kujitokeza kusaidia maendeleeo ya michezo, ikiwemo soka ili kurejesha hadhi ya mche...