Dk. Hussein Ali Mwinyi awaapisha wakuu wa Mikoa wapya.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amewataka Wakuu wa Mikoa wapya wa Zanzibar kuwa na utaratibu maalum unaotambulika wa kusikiliza kero za wananchi pamoja na kuzitafutia ufumbuzi.
Dk. Mwinyi ametoa ushauri huo leo Ikulu jijini Zanzibar katika hafla ya kuwaapisha Wakuu wa Mikoa wapya, watakaohudumu katika Mikoa mitano ya Zanzibar.
Walioapishwa ni Ayoub Mohamed Mahamoud Mkoa Kaskazini Unguja, Rashid Hadid Rashid (Kusini Unguja), Idrissa Kitwana Mustafa (Mjini Magharibi), Salama Mbarouk Khatib (Kaskazini Pemba) pamoja na Mattar Zahor Masoud , mkoa wa Kusini Pemba.
Amesema viongozi hao wana jukumu la kuandaa utaratibu maalum utaowawezesha wananchi kuwasilisha kero mbali mbali zinazowakabili na kuzipatia ufumbuzi wa...