Mjumbe wa Kamat Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Mh. Hemed Suleiman Abdulla zungumza na Wana CCM na Wananchi wa Jimbo la Kiwani
Mjumbe wa Kamat Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Mh. Hemed Suleiman Abdulla alisema Viongozi Wakuu watalazimika kuchukuwa maamuzi magumu katika kuona nidhamu ya Serikali katika kutoa Huduma kwa Wananchi inarejea katika uhalisia wake.
Alisema wakati Serikali inaendelea kupanga safu ya Utendaji katika uwajibikaji wake baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu Wananchi wanapaswa kuunga mkono jitihada hizo ili yale matarajio yao yaweze kufikiwa kwa ufanisi na uharaka uliokusudiwa.
Mh. Hemed Suleiman Abdulla alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na Wana CCM na Wananchi wa Jimbo la Kiwani katika Mkutano Maalum ulioandaliwa wa kumpongeza kwa Kuteuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Hussein Ali Mwinyi kushika wadhifa huo.
Alisema Chama cha Mapinduzi mba...