Riziki haina mja wajipanga kuzalisha vitunguu maji.
KIKUNDI cha Riziki haina mja kinachojishuhulisha na kilimo mchanganyiko, kimesema kuwa baada ya kinakusudia kuendelea na kilimo cha vitunguu maji baada ya kuona zao hilo linakuwa katika eneo lao.
Kikundi hicho kinachotumia eneo la Mjini Ole makaani kwa shuhuli zake za kilimo, msimu huu kimeweza kupata kilo 127 za kitunguu maji zikiwa na thamani ya shilingi Milioni 1.2.
Akitoa taarifa ya kilimo hicho, msimamizi wa kilimo cha Vitunguu Maji katika kikundi hicho, Hamad Khamis Mussa alisema kilimo hicho kilikubali vizuri, ila kilikumbana na changamoto ya mvua wakati wakuvuna na kupelekea vitunguu vingi kuharibika.
“Kwa kiasi kikubwa hili zao linakubali katika eneo letu, awamu hii tumelima na tumeona mafanikio tulioyapata kutokana na mafanikio haya tutaongeza juhudi katika...