Wanafunzi wahimizwa kuendeleza usafi wa mazingira katika maeneo wanayoishi.
HABIBA ZARALI,PEMBA
WANAFUNZI wa skuli mbalimbali zilizojiunga na klabu inayojishughulisha na mazingira Kisiwani Pemba ‘Roots And Shoots’ wametakiwa kutojisahau na badala yake waendeleze kuhifadhi usafi wa mazingira katika maeneo wanayoishi, ili kunusuru kutokea kwa maradhi mbalimbali ya mripuko.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Kisiwani humo Mratibu wa Kanda wa klabu hiyo Zanzibar Ali Juma Ali, alisema usafi wa mazingira ni moja kati ya njia inayoweza kuondosha maradhi ya mripuko yakiwemo ya kuharisha na kipindupindu, ambayo ni hatari kwa maisha ya binadamu.
Alisema ni vyema usafi wa mazingira wanaoufanywa katika skuli zao wauendeleze katika maeneo yao yaliyowazunguka, ili kuweza kwenda sambamba na lengo la klub hiyo la utunzaji wa mazingira na kuleta afya nj...