Wazazi na Walezi kuweni karibu na watoto wenu ili wanapofikwa na vitendo vya udhalilishaji waweze kuwaeleza.
Na Mwashungi Tahir
Imeelezwa kwamba Wazazi na Walezi wametakiwa kuwa karibu na watoto wao ili wanapofikwa na vitendo vya udhalilishaji waweze kuwaeleza baada ya kuonekana vitendo hivyo vinaongezeka Zanzibar kila siku.
Hayo ameyasema Mkaguzi Msaidizi wa Polisi kutoka Makao Makuu ya Polisi Khamis Mwinyi Bakar katika kikao na waandishi wa habari huko katika Ofisi ya Mtakwimu iliopo Mazizini wakati wa ikiwasilishwa takwimu za Ukatili na Udhalilishaji wa Kijinsia kwa wanawake na watoto.
Amesema wazazi wengi wanakuwa na tabia ya kupuuza taarifa za awali za udhalilishaji ambazo wanapewa na watoto wao jambo ambalo linapelekea vitendo hivyo kuzidi kukua zaidi hadi kuwaathiri.
“Tuwe na tabia ya kuwa karibu na watoto wetu ili kuwabaini kwa hara...