Kampuni ya Kimataifa ya Arena yenye Makao Makuu yake Nchini Ujerumani imeonyesha nia ya kutaka kuwekeza Visiwani Zanzibar
Na.Othman Khamis OMPR.
Uongozi wa Kampuni ya Kimataifa ya Arena yenye Makao Makao Makuu yake Nchini Ujerumani inayojishughulisha na Miradi ya Uwekezaji katika Sekta ya Nishati ya Umeme imeonyesha nia ya kutaka kuwekeza Miradi yake Visiwani Zanzibar baada ya kuridhika na mazingira mazuri yaliyopo ya Uwekezaji.
Mwakilishi wa Kampuni hiyo Bwana Souheil Freich aliyeambatana na Uongozi wa Kampuni ya Flagfin yenye Makao Makuu yake Jijini Dar es salaam alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Hemed Suleiman Abdalla hapo Vuga Mjini Zanzibar.
Bwana Souheil Freich alisema alikuwa akifuatilia harakati za Sera na Ilani za Uchaguzi Mkuu uliopita na kuridhika nazo kitendo kilichoipa ushawishi Kampuni yake kutaka kuitumi...