Dk. Hussein Mwinyi azindua Baraza la Kumi la Wawakilishi
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Awamu ya Nane itawekeza kwenye michezo katika kuibua, kuelea na kuendeleza vipaji vya vijana.
Rais Dk. Hussein Mwinyi aliyasema hayo leo katika hotuba yake ya uzinduzi wa Baraza la Kumi la Wawakilishi hafla iliyofanyika huko katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani, nje kidogo ya Jiji la Zanzibar.
Katika hotuba yake hiyo, Rais Dk. Hussein Mwinyi alisema kuwa katika hatua hiyo ya kuekeza kwenye michezo itakwenda sambamba na kukaa na wadau wa soka kutafuta jawabu la kuamsha msisimko wa ligi ya Zanzibar.
“Wakati nakua timu za Zanzibar za Small Simba, Malindi, Mlandege na KMKM zilikuwa ni timu zenye sifa na kuchachafya timu za Bara na zile z...