UVCCM wampongeza DK. Mwinyi.
UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi CCM Tawi la Kichungwani Wilaya ya Chake Chake, wamempongeza Dk.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi, kwa kuchaguliwa kwake huku wakiahidi kuendelea kumuunga mkono katika utendaji wake wa kazi.
Umoja huo umesema Dk.Mwinyi ni kiongozi shupavu na mchapakazi, hivyo watendaji watakaoteuliwa wanapaswa kwendana na kasi yake ya uongozi katika kuijenga Zanzibar mpya yenye maendeleo.
Hayo yameyaeleza na viongozi wa UVCCM Tawi la Kichungwani mjini Chake Chake, wakati alipokuwa katika kikao cha pamoja na vijana wao, cha kujipongeza baada ya kuiweka CCM Tena madarakani.
Katibu wa UVCCM Tawi la Kichungwani Hashil Fadhil Abdulla, alisema dunia nzima inafahamu juu ya ushindi wa Dk.Mwinyi, hiyo inatokana na ufanyaji ...