RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi, amesema serikali atakayoiunda itashirikiana na vyama vya upinzani.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi, amesema serikali atakayoiunda itashirikiana na vyama vya upinzani vilivyokubali na kuridhishwa na matokeo ya urais yaliyotokana na uchaguzi mkuu uliofanyika octoba 28,mwaka huu.
Ahadi hiyo aliitoa wakati akiwahutubia wananchi mara baada ya kuapishwa kuwa rais wa awamu ya nane wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar, katika hafla iliyofanyika uwanja wa Amani Unguja.
Alisema anawapongeza wagombea wa vyama vya upinzania waliokubali matokeo ya uchaguzi na kuheshimu maamuzi ya wananchi na ninatoa ahadi ya kushirikiana nao katika serikali atakayounda.
“Ndugu zangu ninawapongeza wagombea wenzangu kwa nafasi ya urais ambao wameyakubali matokeo ya uchaguzi na kuheshimu maamuzi ya wananchi na ninatoa ah...