DK Mwinyi anena Kiwani.
IMEANDIKWA NA HABIBA ZARALI NA HAJI NASSOR, PEMBA.
MGOMBEA urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema iwapo wananchi wa Zanzibar watampa ridhaa ya kushika nafasi hiyo, ataimarisha huduma za afya, ili wananchi wapate uhakika wa matibabu.
Dk. Mwinyi ameyasema hayo uwanja wa mpira Jimbo la Kiwani wilaya ya Mkoani, mkoa wa kusini Pemba, kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni wa chama hicho, uliokuwa na lengo la kuwanadi wagombea wa CCM.
Alisema, hayo ndio kipaumbele chake cha kwanza mara atapomaliza kuapishwa, kwani mambo hayo ni miongoni mwa mambo muhimu kwa wananchi.
Alisema moja ya dhamira yake ya kugombea nafasi hiyo, ni kuwatumikia wananchi kwa moyo wa dhati, na ndio maana anakusudia kuimrisha huduma za afya.
Alisema ata...