Wednesday, October 30
Marcus Rashford amekuja na kampeni kuitaka Serikali ya Uingereza kuidhinisha ongezeko la bajeti ya huduma ya chakula kwa watoto mashuleni.
Michezo

Marcus Rashford amekuja na kampeni kuitaka Serikali ya Uingereza kuidhinisha ongezeko la bajeti ya huduma ya chakula kwa watoto mashuleni.

  Mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford amekuja na kampeni mpya ya kutaka Serikali ya Uingereza kuidhinisha ongezeko la bajeti ya huduma ya chakula kwa watoto mashuleni ili kupunguza baa la njaa miongoni mwao. Huu ni mlolongo wa vitendo vya kiungwana kwa mchezaji huyo mara baada ya dunia kutambua mchango wake katika kusaidia kaya mbalimbali nchini Uingereza kwa kuwapa huduma mbalimbali ikiwemo chakula kipindi cha janga la ugonjwa wa COVID19. Katika kampeni inayoendeshwa na mchezaji huyo mwenye miaka 22 ametaja mapendekezo matatu ambayo ni pamoja na ongezeko la idadi ya watoto milioni moja na laki tano wanaotakiwa wapate chakula ambao ni kuanzia wenye umri wa kati ya miaka 7 hadi 16. Vilevile ongezeko la utoaji misaada hususani kipindi cha sikukuu kwa kutoa chakula...
DK. Shein azindua barabara Ole-Kengeja.
Kitaifa

DK. Shein azindua barabara Ole-Kengeja.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, amewataka wananchi na watumiaji wa brabara ya Ole- Kengeja, kufanya kila njia ili kuhakikisha wanaitunza kwa nguvu zao zote, barabara hiyo ili idumu kwa muda mrefu. Dk. Shein ameeleza hayo uwanja wa mpira Kengeja wilaya ya Mkoani Pemba, alipokuwa akizungumza na wananchi wa mikoa mwili ya Pemba, mara baada ya kuzindua barabara hiyo mpya yenye urefu wa kilomita 35. Alisema barabara ndio kichecheo kikubwa cha maendeleo ya wananchi kwa kule kuitumia kwa shughuli zao mbali mbali iwe ni usafirishaji mazao, hivyo suala la kuitunza ni jambo la lazima. Alisema, ujenzi wa barabara hiyo umetumia fedha nyingi, hivyo hakuna budi kuona upo umuhimuwa na ulazima wa kuitunza kwa wananchi, ili itumike na k...
DK. Shein azindua BOHARI ya dawa Pemba.
Kitaifa

DK. Shein azindua BOHARI ya dawa Pemba.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, amesema kujengwa kwa bohari ya kuhifadhia dawa kisiwani Pemba, litaondosha tatizo la uagiziaji dawa Unguja na kwamba Hospitali na vituo vya afya vyote Pemba vitachukuwa dawa katika bohari hiyo kwa wakati muwafaka. Alisema hayo ni mafanikio makubwa ambayo hayajawahi kufikiwa, hivyo wananchi na watendaji wanapaswa kulitunza na kulithamini, ili bohari hiyo inadumu kwa muda mrefu na kukidhi mahitaji wa dawa. Rais Dk.Shein aliyaeleza hayo mara baada ya kuzindua rasmi bohari ya kuhifadhia Dawa, huko Vitongoji Changuo Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kuisni Pemba. Aidha Dk Shein aliahidi kufanya kila linalowezekana, kuona dawa muhimu zinapatikana katika haospitali na vituo vyote vya afya, kwamba serikali ime...
Kuweka mazingira safi ni njia ya kujikinga na maradhi yakiwemo ya mripuko. Waziri Hamad.
Kitaifa

Kuweka mazingira safi ni njia ya kujikinga na maradhi yakiwemo ya mripuko. Waziri Hamad.

  Waziri wa Afya Zanzibar Mh. Hamad Rashid Mohammed amewataka wananchi kuongeza juhudi katika kuweka mazingira yao safi na salama ili kuepuka kushambuliwa na maradhi yatakayopelekea kuzorotesha afya zao na kurudi nyuma kimaendeleo. Muheshimiwa Hamad ametoa wito huo wakati alipokuwa akizungumza na wananchi katika maadhimisho ya siku ya kunawa mikono duniani huko katika Ukumbi wa  Samail Gombani Kisiwani Pemba. Mh. Hamad amesema ili mafanikio zaidi yaweze kupatikana ni lazima wananchi wawe katika hali ya usafi wa mazingira yao huku wakidumisha amani iliyopo ili kila mmoja aweze kupata nafasi ya kufanya kazi kwa ufanisi. “siku zote uchafu ndio ambao unasababisha maradhi na watu wengi huugua kutokana na uchafu” alisema Mh. Hamad. Amesema mara nyingi kunapotokea maradhi ...
DK. Shein anena Micheweni.
Kitaifa, Siasa

DK. Shein anena Micheweni.

MAKAMU mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar, Dk.Ali Mohamed Shein amesema kazi kubwa iliyopo mbele inapaswa kufanywa na wanaccm, kwa kuhakikisha wakakirudisha tena madarakani chama cha Mapinduzi na dhambi ya wanahubiri ugomvi ni kuwanyima kura. Alisema uongozi hautaki mzaha au kujaribu, kwani wanaCCM wako makini sana ndio maana wakakamilisha utekelezaji wa ilani ya CCM ya miaka mitano iliyopita, na kufanikiwa katika mambo mengi ya maendeleo hata yakipimwa kwa kutumia mizani. Makamu huyo mwenyekiti wa ccm Zanzibar, ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi, aliyaeleza hayo katika uwanja wa Shamemata Micheweni, wakati akiwahutubia wananchi na wanaccm wa wilaya hiyo. Akizungumzia suala la Mapinduzi matukufu ya zanzibara ya 1964, ndio yaliyoleta uko...