Wednesday, October 30
Wajue ndege wenye upepo.
Biashara, Kitaifa

Wajue ndege wenye upepo.

  Wanyama 10 walio na kasi zaidi duniani Baadhi ya wanyama hao huruka angani, wengine huogelea baharini na wengine hukimbia ardhini kulingana na mtandao wa OneKindPlanet unaoangazia elimu ya wanyama. Hawa ni wanyama 10 bora walio na kasi zaidi duniani Sungura wa Hudhurungi CHANZO CHA PICHA,DE AGOSTINI PICTURE LIBRARY Ana miguu mirefu ya rangi nyeusi inayomuwezesha kukimbia kwa kasi ya kilomita 77 kwa saa, kasi sawa na mbwa mwitu mwekundu. Nyumbu wa Samawati
 CHANZO CHA PICHA,HOBERMAN COLLECTION/GETTY Nyumbu wa buluu, Springbok na gazelle wote wanaweza kukimbia kasi ya kilomita 80 kwa saa karibu sawa na kasi ya simba Samaki aina ya Marlin CHANZO CHA PICHA,BBC/TWITTER Marlin anaweza kuogelea kwa kasi ya kilomita 80 kwa saa, ak...
Abdulla Mzee Mkoani Pemba yakabidhiwa  Mashine ya kupimia Damu kwa uchunguzi wa maradhi mbali mbali.
Kitaifa

Abdulla Mzee Mkoani Pemba yakabidhiwa Mashine ya kupimia Damu kwa uchunguzi wa maradhi mbali mbali.

  Picha na – OMPR – ZNZ.   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema upatikanaji wa Vifaa vya Kisasa vya Afya katika Hospitali mbali mbali Nchini ni mwanzo mwema wa Zanzibar kukomboka katika utoaji wa huduma bora za Afya kwa Wananchi wake. Alisema mfumo uliokuwa ukitumika wa baadhi ya Wagonjwa kuwasafirisha Tanzania Bara na wengine nje ya Nchi mbali ya kutumia gharama kubwa za Fedha lakini pia ulikuwa ukihatarisha afya za wale wagonjwa wanaosafirishwa wakati tayari wanasumbuliwa na Maradhi. Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati akiukabidhi Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Abdulla Mzee Mkoani Pemba Mashine ya kupimia Damu kwa uchunguzi wa maradhi ya Moyo, Figo, Maini pamoja na vitakasa mikono vilivyotolewa na Mfanyabiashara Maar...
Mtoto wa miezi saba arudi kwa mama yake.
Kitaifa, Sheria, Wanawake & Watoto

Mtoto wa miezi saba arudi kwa mama yake.

  NA MARYAM  SALUM, PEMBA.   MTOTO  wa miezi saba aliyekosa  kunyonya maziwa ya mama yake  kwa muda wa wiki mbili, mahakama  ya Mkoa Chake  chini ya hakimu Luciano  Makoye  Nyengo, imefanikiwa kumrejesha mtoto  huyo kwa mama yake,  ili aweze kupata haki yake hiyo. Mahakama iliesema kuwa chanzo cha mtoto huyo kukosa haki yake hiyo, ni baada ya baba mzazi wa mtoto huyo kuamua kumchukuwa kwa muda wa wiki mbili na kwenda kuishi nae kwenye  familia yake. Mahakama  hiyo  ilisema kuwa ilipokea ombi hilo kutoka kwa mama mzazi wa mtoto huyo, Zulfa Hassan Ussi mwenye miaka 21, mkaazi wa Machomane, na kudai  mahakama hapo kuwa mtoto wake wa miezi saba  amechukuliwa na mumewake na kuishi nae katika  sehemu nyengine. “Muheshimiwa nimekuja  katika  mahakama yako kuleta om...
TASAF yawakutanisha waandishi Tanga.
Kitaifa

TASAF yawakutanisha waandishi Tanga.

  NA ABDI SULEIMAN, TANGA.     WAANDISHI wa habari wameshauriwa kuwashajihisha walengwa wa mpango wakunusuru kaya masikini Tanzania, kutumia rasilimali zozote zinazotolewa na mfuko wa maendeleo ya jamii Tanzania (TASAF)kuweza kuboresha maisha yao. Ushauri huo umetolwa na Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Judika Omra, wakati alipokuwa akifungua kikao kazi cha kuwajengea uwelewa, waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya Tasaf, kimewashirikisha waandishi wa habari kutoka Dar Esalam, Morogoro, Unguja na Pemba na kufanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga. Alisema waandishi wandishi wahabari ni watu muhimu sana, katika kuelimisha jamii katika masuala mbali mbali hivyo, wanapaswa kuwa mabalozi wazuri kwa jamii...
Wanafunzi kushirikishwa katika kongamano la Siku ya Maafa dunaini.
Kitaifa

Wanafunzi kushirikishwa katika kongamano la Siku ya Maafa dunaini.

  AFISA Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba, Mohamed Nassor Salima amesema kushirikishwa kwa wanafunzi katika kongamano la Siku ya Maafa dunaini, litakuwa ni mwarubaini wa majanga maengine kutokea katika jamii. Alisema hilo litatendeka, pale wanafunzi hao watakapoifikisha elimu ya maafa katika jamii iliyowazunguruka, kwa kufuata mikakati na kanuni za kukabiliana na maafa. Mdhamini huyo aliyaeleza hayo wakati alipokuwa akifungua kongamano la wanafinzi, kuelekea siku ya maafa duniani, lililofanyika katika skuli ya Mdungu Sekondari. “Wanafunzi hawa ni vyanzo vizuri vya kufikisha ujumbe kwa jamii, watawaelimisha wazazi wao, marafiki zao elimu itaweza kuenea kwa wingi”alisema. Akizungumzia umuhimu wa Makongamano hiko kwa wanafunzi, alisema litaweza kuw...