PBZ Tawi la Wete imeadhimisha siku ya wateja.
BENK ya watu wa Zanzibar PBZ Tawi la Wete, imeadhimisha siku ya wateja wa Benk, kwa kujumuika na wateja wao na kuwashukuru kwa kuendelea kuwa na imani na benk yao.
Tawi hilo lenye maskani yake bopwe Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, imeadhimisha siku hiyo kwa ukataji wa keki na kujumuika na wateja wake.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, kaimu meneja wa benk hiyo Ahmed Abubakar Mohd, aliwashukuru wateja wa benk hiyo kwa kuendelea kuwa na imani na benk yao, na kuahidi kuwahudumikia kwa hali na mali.
Alisema benk hiyo imekua ikitoa huduma mbali mbali kwa jamii, ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na zenye uhakika, kuhakikisha uchumi unakuwa na kufikia uchumi wa buluu.
“Sisi leo tumeona tuungane na wananchi wetu katika kuadhimisha siku ya wateja wa mabenk...