Meneja kampeni Mkoa kusini Pemba awanadi wagombea wa CCM wa jimbo la Ole.
MENEJA kamopeni za Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Pemba, Mohamed Aboud Mohamed amewataka wananchi wa jimbo la Ole Wilaya ya Chake Chake, kuitumia bahati ya kipekee ya kupata viongozi wenyenia ya kuwatumikia wananchi wajimbo hilo
Alisema jimbo la ole katika miaka mingi iliyopita, lilikuwa chini ya utawala wa chama cha CUF, huku wananchi wakikosa maendeleo waliokuwa wakiahidiwa na viongozi walioowachagua.
Meneja huyo aliyaeleza hayo wakati alipokuwa akiwanadi wagombea ubunge, uwakilishi na udiwani wa jimbo hilo, katika mkutano wa hadhara wa kampeni zilizofanyika unja wa mpira Vumba Vitongoji.
Alisema wananchi wa jimbo la Ole wanakila sababu kuwachagua wagombea wa wote wa CCM, katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu ili viongozi hao waweze kuwatumikia.
“Kazi yenu ni kwenda k...