Dk. Hussein Ali Mwinyi :Nitasimamia uwajibikaji na watakoshindwa nitawawajibisha.
NA HAJI NASSOR, PEMBA
NGOMBEA urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema iwapo wananchi wa Zanzibar watampa ridhaa ya kushika nafasi hiyo, atahakikisha, anasimamia uwajibikaji na watakoshindwa atawawajibisha, ili mafanikio ya kweli yapatikane.
Alisema, hayo ndio kipaumbele chake cha kwanza mara atapomaliza kuapishwa, kwani mambo hayo ni miongoni mwa yanadhoofisha kwa kiasi kikubwa maendeleo ya jamii.
Mgombea huyo wa urais, aliyasema hayo Jimbo la Gando wilaya Wete mkoa wa kaskazini Pemba, alipokuwa akizugumza na mamia ya wanaccm na wananchi wengine, kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni wa chama hicho.
Alisema kuwa, serikali atakayoiongoza hatopenda hata kidogo kuona ndani yake, mna watendaji wasiopenda...