Wagombea CCM Jimbo la Chonga wanadi sera zao.
WAGOMBEA Ubunge na Uwakilishi Jimbo la Chonga Wilaya ya Chake Chake, kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) wamesema iwapo wananchi watawapa ridhaa ya kuongoza jimbo hilo, watahakikisha wanashirikiana katika kupeleka maendeleo pamoja na kutatua kero zote zainazowakabili wananchi wa jimbo hilo.
Wagombea hao wamesema kuwa kwa sasa wanasubiri ridhaa za wananchi tu, ili kuanza harakati zakulibadilisha jimbo hilo ambalo kwa miaka mingi lilisahauliwa na viongozi wa jimbo waliokuwepo.
Wakizungumza katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni za jimbo hilo, huko katika uwanja wa Mpira wa Skuli ya Pujini Wilaya ya Chake Chake, zikiongozwa na meneja wa Kampeni za CCM Mkoa wa kusini Pemba Mohamed Aboud Mohamed.
Mgombea Ubunge wa jimbo hilo Juma Mohamed Juma, alisema iwapo atapata ridhaa ya kuwa ...