VIDEO: Wagombea jimbo la Kiwani wanadi sera zao.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kiwani katika Wilaya ya Mkoani ndugu Rashid Abdalla Rashid amewataka wananchi wa Jimbo hilo kumchagua na kuendelea kukipigia kura Chama cha Mapinduzi ili kiweze kuwaletea maendeleo wazanzibar na Watanzania kwa ujumla.
Ndugu Rashid ameyasema hayo huko Mwambe wakati wa uzinduzi wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi katika jimbo la Kiwani.
Amesema katika uongozi wa awamu ya saba inayomalizia kuna miradi mingi ya maendeleo imeekezwa kwa ajili ya kuwaondoshea kero wananchi hivyo ni vyema kuendelea kukiweka madarakani chama cha mapinduzi ili wananchi wazidi kunufaika na maendeleo hayo.
Naye mgombea wa uwakilishi wa jimbo la Kiwani ndugu Mussa Foum Mussa amesema katika kipindi kilichopita wakati akiwa mwakilishi wa jimbo hilo alifanikiwa kusimamia upatiukan...