Maalim Seif kukuza pato la mwani akiingia Ikulu tu
MGOMBEA wa urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya Chama cha ACT- Wazalendo maalim Seif Sharif Hamad, amesema endapo wananchi wa Zanzibar watamchaguwa na kumuweka madarakani, atahakikisha wakulima wa mwani wanapata faida kwa kuweka bei nzuri ambayo itakidhi machungu ya kilimo hicho.
Maalim Seif aliyaeleza hayo huko Tumbe wilaya ya Micheweni Pemba, wakati akizungumza na wakulima wa mwani pamoja na wavuvi wa eneo hilo, katika ziara yake kisiwani humo.
Alieleza kuwa, wanunuzi wa mwani wanakuwa wanawadhulumu wakulima kwa kununua zao hilo kwa bei ya chini ya shilingi 600 kwa kilo moja.
“Tukingia madarakani nitahakikisha Serikali yangu inawahudumia wakulima wa mwani, kwa kuwapatia vyombo ambavyo vitafika maji makubwa, ili waweze kulima mwani bora wa Cotonee ambao unabei kubwa katika...