Wednesday, January 8
PPC yaanza kuvitangaza vivutio vya Utalii Pemba.
hifdhi na utalii, UTLII

PPC yaanza kuvitangaza vivutio vya Utalii Pemba.

Yasema sababu na Uwezo wa kufanya hivyo wanao Kuunga mkono kauli ya Rais wakiwa kama waandishi  na Wananchi ni wajibu wao HABIBA ZARALI ,PEMBA Mkuu wa wilaya ya Micheweni Mgeni Khatib Yahya ameahidi kuendelea kutowa elimu kwa wananchi wa Wiaya hiyo juu ya umuhimu wa Utalii na kuboresha vivutio vya utalii ndani ya maeneo yao. Alitowa ahadi hiyo wakati alipokuwa akizungumza na wanachama wa Klabu ya waandishi wa habari Pemba ‘PPC’ katika mahojiano maalum yaliyofanyika katika maeneo ya makumbusho ya Haroun site , Chwaka Tumbe wilayani humo. Alisema katika wilaya ya Micheweni kumebarikiwa na vivutio vingi vya utalii vinavyoendelea kukuwa siku hadi siku jambo ambalo ni faraja kubwa kwa wananchi na Serikali kwa ujumla katika kukuza Uchumi. “Zamani wilaya ya Micheweni suala la...
Akinamama wenye VVU wapumzike baada ya kujifungua-Dk. Rahila
afya

Akinamama wenye VVU wapumzike baada ya kujifungua-Dk. Rahila

NA ZUHURA JUMA, PEMBA AKINAMAMA wanaoishi na Virusi vya Ukimwi wametakiwa kupata mapumziko baada ya kujifungua, ili wapate kuimarika kiafya pamoja na mtoto wake, huku akifuata maelekezo ya daktari wakati gani kwake anaweza kubeba mimba. Aizungumza na mwandishi wa habari hizi, Msimamizi wa Vituo vya kutoa huduma kwa watu wenye VVU Dk, Rahila Salim Omar alisema, mwili unapotoa kiumbe unahitaji kujirejesha tena katika hali ya kawaida na ndipo uweze kubeba mimba nyengine. Alisema kuwa, wakati wa ujauzito kinga ya mwili inashuka, kwa hiyo uwezekano wa kupata maambukizi mengine unakuwa ni mkubwa kiasi kwamba anaweza kupata maambukizi mengine yatakayoweza kumsababishia mtoto kupata VVU. Alifahamisha kuwa, afya ya mama huyo inakuwa bado haijarudi katika hali yake ya kawaida, hivyo ...
KOICA YAKABIDHI DAHALIA LA WANAWAKESKULI YA TUMBE
ELIMU

KOICA YAKABIDHI DAHALIA LA WANAWAKESKULI YA TUMBE

BAKAR MUSSA ,PEMBA WAZIRI wa Kilimo , Umwagiliaji na mali asili Zanzibar , Shamata Shaame Khamis ameipongeza Serikali ya Korea Kusini  kupitia Shirika lake la KOICA ( Korea International Cooperative Agency) kwa juhudi zake wazozichukuwa za kuisaidia Serikali ya Mapinduzi Zanzibar misaada mbali mbali ikiwemo Elimu. Alisema Elimu ndio kitu muhimu katika maisha ya mwanaadamu kwani huwezi kufanya jambo lolote bila ya kuwa na elimu na ndio Mwaasisi wa Mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964 na Rais wa Kwanza wa Zanzibar hayati Abeid Aman Karume akatangaza kuwa Elimu itolewe bila ya malipo (Elimu bure). Alieleza hayo huko katika Skuli ya Sekondari Chwaka Tumbe , kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Zanzibar , Tabia Maulid Mwita wakati wa hafla ya Uwekaji ...
ZIC Yazindua Mpango wa Mabadiliko ili Kuchochea Utoaji Huduma kwa Wateja
Biashara

ZIC Yazindua Mpango wa Mabadiliko ili Kuchochea Utoaji Huduma kwa Wateja

Mukrim mohammed-Zanzibar Shirika la Bima la Zanzibar (ZIC) limezindua mpango wake mpya wa kubadili muonekano na taswira yake kijamii na kibiashara hatua ambayo inalenga kuakisi ukuaji wa shirika hilo sambamba maboresho ya huduma zake kwa wateja. Hatua hiyo mkakati inahusisha mfululizo wa mabadiliko chanya yanayohusisha muonekano mpya wa nembo ya shirika hilo, muonekano wa nyaraka rasmi za ofisi, maboresho ya huduma kwa wateja sambamba na mabadiliko ya muonekano wa ofisi za shirika hilo. Hafla ya uzinduzi rasmi wa muonekano mpya wa ZIC imefanyika leo Zanzibar, ikiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Dkt. Saada Mkuya Salum. Pamoja na Waziri Mkuya pia walikuwepo  Naibu Kamishna wa Bima Tanzania, Khadija Issa Said, Balozi wa Bima nchini  Wanu Hafidh A...