Kilio cha upatikanaji wa maji safi na salama bweni la skuli ya Madungu Sekondari chamaliza.
NA AMINA AHMED-PEMBA.
KWA zaidi ya Miezi mitatu na siku kadhaa sasa hofu ya usalama wa afya kwa baadhi ya wanafunzi wanaokaa katika bweni Skuli ya Madungu sekondari imeondoka hii ni baada ya kupatikana huduma ya maji safi na salama muda wote skulini hapo, sambamba na kuwepo kwa utaratibu maalum wa uzolewaji wa taka katia eneo wanalotumia kutupa taka mbali mbali.
Wakizungumza na habari hizi baadhi ya wanafunzi wanaokaa katika bweni skulini hapo wamesema kuwa hali ya kuishi kwa wasi wasi na hofu ya maradhi kwa sasa imeondoka hali ambayo imesaidia kuzidisha umakini zaidi katika masomo yao.
Aidha wamemshukuru mwandishi wa habari hizi kwa jitihada aliyochukua katika kuhakikisha suala hili linakuwa sawa na kupatiwa ufumbuzi.
"Nilipoona maji yanatoka siku iyo hayajafungwa...