PPC wamlilia Magufuli.

 

NA ABDI SULEIMAN.

KLABU ya Waandishi wa habari Kisiwnai Pemba (PEMBA PRESS CLUB) imesema Tanzania imompoteza kiongozi shupavu aliyekuwa mstari wambele kutetea haki za wanyonge na walemavu.

Hayo yameelzwa na Mwenyekiti wa Klabu hiyo Bakari Mussa Juma wakati alipokua akisaini kitabu cha Maombolezo ya aliyekua Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Hayati Dkt.Jaohn Pombe Magufuli, huko katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba.

Mwenyekiti huyo alisema Rais Magufuli alikuwa ni kiongozi Shupavu na mjasri katika kutetea haki za walemavbu, wanyonge, mama ntilie na vijana.

Alisema Tanzania imepata na msiba mkubwa, msiba ambao pengo lake kuzibika kwa haraka haraka, huku akiwataka wananchi na watanzania kuendelea kutulia na kuvumilia na kudumisha amani na utulivu uliopo.

“Hayari Rais Dkt. Magufuli aliweza kujitolea Roho yake kwa ajili ya kuwasaidia wanyonge, alifika hadi kupunbuza mshahara wake kwa mwezi anao lipwa, ili nchini iweze kunyanyuka na kujitengenea wenyewe katika Nyanja mbali mbali”alisema.

Aidha alisema katika kuhakikisha anaenziwa kwa vitendo, lazima watanzania kutekeleza kwa vitendo yale yote aliyokuwa amiyakemea, ikiwemo suala zima la zulma, wizi wa mali za Umme, Rushwa.

Hata hivyo aliwataka waandishi wa habari nchini, kuhakikisha wanatumia kalamu zao katika suala zima la kuhubiri amani, pamoja na kukemea yale yote aliyokuwa hayapendi hayati Rais John Magufuli.

Kwa upande wake mwandishi wa habari Masanja Mabula Shari, alisema kifo cha Magufuli ni pigo kubwa kwa Tainzania, Africa na Dunia kwa ujumla.

Alisema Rais Magufuli aliweza kuisimamisha dunia kwa muda, kufuatia Tanania kuingia katika suala la uchumi wa kati, hali iliyopelekea baadhi ya nchi kuanza kuja Tanzania kujifunza mambo mbali mbali.

Aidha aliwataka waandishi wa habari Pemba, kuhakikisha wanatumia kipindi hiki cha maombelezo kwa kuelezea jamii mambo ambayo yamefanywa na Hayati Mzee Magufuli.

Kwa uonde Seif Shaban mkaazi wa Wawi, alisema Hayati Rais Dkt.Magufuli aliweza kuibadilisha Tanzania kwa kiasi kikubwa katika Nyanja mbali mbali za kiuchumi na kijamii.

Hata hivyo aliwataka wananchi na watanzania kufuata nyayo zake katika kuhakikisha Tanzania inasimama na inaendelea kupiga vita suala zima la Rushwa.

Naye Aziza Yussuf Salehe, alisema Rais Magufuli aliweza kupiga vita suala zima la ukabila, udini na ubaguzi wa aina yoyote na kuwafanya watanzania kuwa wamoja.

Katibu Tawala Mkoa wa Kusini Pemba Amour Hamad Saleh, aliwataka watanzania kumpatia mashirikiano Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suhulu Hassan ili kuweza kuyatekeleza yote yaliyoachwa na hayati Rais Dkt. Magufuli.